RUNGU la adhabu linawasubiri wachezaji wa timu ya soka ya Simba, Hamisi Kiiza na Juuko Murshid ambao hawajaungana na wenzao mazoezini hadi sasa.Wachezaji hao raia wa Uganda walikuwa kwao kuiwakilisha timu yao ya taifa ‘The Cranes’ kwenye mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2017 dhidi ya Burkina Faso na walitakiwa kurudi baada ya mechi hiyo iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zilisema jana kuwa wachezaji hao wamekaidi agizo la uongozi wao ambapo walitakiwa kuripoti baada ya mechi yao hiyo ya kimataifa mwishoni mwa wiki iliyopita.“Mpaka sasa hawajajiunga na wenzao na hakuna taarifa zozote za kwa nini hawajarudi nchini,” alisema mtoa taarifa wetu, ambaye aliomba jina lake lisitajwe.Aisema tayari wachezaji hao wameshaandikiwa barua ya kuwataka kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kuchelewa kuungana na wenzao katika maandalizi ya mechi za Ligi Kuu na zile za Kombe la FA.“Barua tumewapelekea wao na tumepeleka kwa Shirikisho la Soka Uganda (Fufa), hivyo tunasubiri maelezo yao na tutachukua hatua, hatuwezi kuvumilia utovu wa nidhamu wa hali hii,” alisema.Kocha Mkuu wa timu hiyo ambaye pia ni raia wa Uganda, Jackson Mayanja alikaririwa akisema amefanya juhudi za kuwasiliana na kocha wa Uganda, Milutin Sredjovick ‘Micho’ kujua kilichowakwamisha wachezaji hao, lakini alionesha kushangaa Kiiza na Murshid kushindwa kuripoti.“Sasa nasubiri uongozi utachukua hatua gani lakini nimewasiliana na kocha Micho naye alishangaa kusikia wachezaji hao hawapo na timu,” alisema.Tangu kuwasili kwa Mayanja amekuwa akisisitiza nidhamu na tayari wachezaji wawili Hassan Isihaka na Abdi Banda wameshaadhibiwa.Alipoulizwa jana kuhusiana na habari hizo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema atafutwe baadaye, lakini alipotafutwa baadaye simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.
Latest News
Loading...
Kocha. Yanga imenoga Pemba
Related Posts:
Liverpool yakamilisha usajili wa Chamberlain Ikiwa ni siku ya mwisho ya dirisha la usajili nchini Uingereza klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain kutoka katika klabu ya Arsenal kwa kiasi cha pauni milioni 35.Chamberlain … Read More
“Natarajia kuwa na timu bora mara mbili ya Serengeti Boys iliyopita”-Kocha Milambo Na Thomas Ng’itu Kocha Oscar Milambo wa Serengeti Boys ametamba kutengeneza kikosi kipya cha Serengeti Boys na kuwa imara zaidi ya kikosi cha mara ya kwanza. Milambo akipiga stori na ShafihDauda.co.tz alifunguka wamean… Read More
BREAKING NEWS: Kamati ya Nidhamu TFF Yawatolea Tamko Msuva, Chirwa NA Kaseke Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemkuta na makosa ya utovu wa nidhamu aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga anayekipiga nchini Morocco, Simon Msuva ambaye imempa onyo kali la barua.Mbali na Msuva, wengine… Read More
VIDEO: Mourinho kalipa kisasi kwa Guardiola September 10 2016 ilikuwa siku ya kihistoria kwa makocha waliokuwa na upinzani tokea wakiwa katika Ligi Kuu Hispania Jose Mourinho na Pep Guardiola, wakati huo walikuwa wanakutana kwa mara ya kwanza wakiwa wanafundish… Read More
Wakala aondoa utata wa safari ya Farid Musa (Azam FC) Hispania Wakala wa kiungo wa Azam FC, Farid Mussa anayesimamia dili lake la kwenda kucheza soka nchini Hispania, John Solzano, amemaliza utata uliopo juu ya safari yake. Solzano ambaye ni raia wa Hispania, amesema kila kitu kimeka… Read More
0 comments:
Post a Comment