Latest News
Loading...
Tetemeko laporomosha majumba na kusababisha maafa makubwa.
Tetemeko lingine baya la ardhi, limegonga maeneo ya katikati mwa Italia, mahali ambapo watu 300 waliuwawa mwezi Agosti mwaka huu.
Idara ya Seisomologia nchini Italia inakadiria kuwa tetemeko hilo lilikuwa lenye nguvu ya 6.5 katika vipimo vya Richa, tetemeko baya zaidi tangu lilile lililoitetemesha Italia mwaka 1980, iliyowauwa watu elfu 2,400.
Tetemeko la sasa limeporomosha jengo la kale la kanisa la mtakatifu Benedict mjini Norcia, pale wamonaki na watawa walikuwa wamekusanyika.
Meya wa mji ulioko karibu wa Ussita- Marco Rinaldi, amesema kuwa alikodolea macho kuzimu, kwani kila kitu kilichomzunguka kiliporomoka akitazama.
Duru zasema kuwa mji wa Amatrice -ambao uliharibiwa na tetemeko la mwezi Agosti, limeharibiwa tena zaidi.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kwamba watu tisa wamejeruhiwa lakini taarifa kuhusu vifo bado hazijatolewa.
Kitovu cha tetemeko hilo lilikuwa kusini mashariki mwa mji wa Perushia.
Mtu aliyevalia kama mti akamatwa Marekani
Mwanamume mmoja nchini Marekani, ambaye ameanza kufahamika kama "binadamu mti", alikamatwa baada yake kuvuka barabara akiwa amevalia kama mti.
Asher Woodworth, kutoka jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka kizuizini.
Asher baadaye aliachiliwa huru na polisi.
Aliambia BBC kwamba alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale alipokabiliwa na maafisa wa polisi.
Yeye ni mwigizaji mjini Portland, Maine.
Anasema: "Nilipata wazo hili nilipokuwa natafakari sana siku moja."
Anasema alikuwa anataka tu kuwashangaza watu kwa mavazi yake na kuwafanya "watafakari upya kuhusu matarajio yao".
Alikuwa ametumia matawi ya miti ya aina mbalimbali na anasema ilimchukua yeye na rafiki yake saa kadha kukamilisha vazi hilo.
Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa "yananukia".
Lakini mbona akaamua kuvalia matawi ya miti?
"Huwa nahisi nina uhusiano wa karibu na miti, naipenda sana," aliambia.
Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini.
Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.
Majina ya watu 4 matajiri zaidi Tanzania
Uchumi mkubwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unategemea zaidi kilimo kwa takriban asilimia 25 ya pato la taifa na asilimia 85 bidhaa zinazouzwa nje ya nchi. Aidha, Tanzania ina madini kama dhahabu, almasi, makaa ya mawe, uraniamu, chuma, shaba, Tanzanite na mengine lukuki.
Toka kuaga sera za kijamaa katikati mwa miaka ya 1980, ambako pia Mwalimu Nyerere aling’atuka kupisha utekelezaji wa sera za kibepari, Tanzania imetengeneza matajiri wengi. Katika makala hii fupi, tumekusanya majina ya Watanzania wanne, ambao ndio matajiri wakubwa zaidi nchini Tanzania, kwa mujibu wa jarida maarufu duniani la Forbes.
4) Reginald Mengi – Thamani: $560 Million
Bwana Reginald Mengi ni mmiliki wa moja ya kampuni kubwa inayomiliki vyombo vya habari ya IPP Media Group, yenye magazeti 11, stesheni za redio na TV na mitandao ya intaneti.
3) Said Salim Bakhresa – Thamani: $575 Million
Umri wake ni miaka 65, na yeye alianza mwenyewe mpaka kufikia hapo. Mfanyabiashara huyu ameanzisha Azam TV, yenye mfumo wa kulipia chaneli za TV Afrika ya Mashariki. Aliacha shule akiwa na miaka 14 na kuanza kuunza Mix (Urojo) na baadae kufungua mgahawa mdogo eneo la Livingstone Kariakoo jijini Dar Es Salaam, na kisha kuhamia katika biashara ya mazao ya kilimo. Katika miongo minne iliyopita ameongeza mauzo yake kwa dola za kimarekani milioni 750, na kuifanya Bakhresa Group kuwa moja ya kampuni kubwa Afrika ya Mashariki kwa kuwa na wafanyakazi zaidi ya 5,000 na kujikita zaidi kwenye bidhaa za vinywaji na chakula, Upakiaji wa bidhaa, huduma za feri na Mafuta ya Petroli na usafirishaji.
2) Rostam Aziz –Thamani: $1 Billion
Mnamo mwezi Mei mwaka 2014 aliuza hisa zake 17% alizokuwa akimiliki katika kampuni ya Vodacom. Vile vile ana miliki kampuni Caspian Mining, inayojihusisha na uchimbani wa madini kwenye kampuni kubwa kama BHP Billiton na Barrick Gold. Kampuni hiyo ya Caspian Mining pia inamiliki sehemu kubwa ya ardhi yenye uwezekano wa kuwa na madini kama dhahabu, chuma na shaba hapa Tanzania. Aidha, Rostam ana hisa katika Bandari ya Dar es salaam ambapo yuko pamoja na Hutchison Whampoa na ana miliki sehemu ya ardhi kubwa hapa Tanzania, Dubai, Oman na Lebanon.
1) Mohammed Dewji – Net Worth: $1.3 Billion
Ana umri wa miaka 40, na ndio mdogo kuliko matajiri 50 wa Afrika yote kwa mfululizo wa miaka 3 sasa, ana miliki 75% ya kampuni ya METL Group, inayohusika na viwanda nchini humu iliyoanzishwa na Baba yake. Kizuri kuhusu Mohammed Dewji aliibadisha nyumba ya kufanyia manunuzi ya bidhaa za kilimo kuwa kiwanda cha uzalishaji.
Kwa Mara ya Kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Kutembelea Nchini Kenya....
Kwa mara ya kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, atazuru taifa jirani la Kenya hapo kesho Jumatatu.
Ziara ya Magufuli nchini humo, inatukia wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegea.
Kwenye ajenda ya ziara hiyo rasmi ya kiserikali, kati yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili, kwani Rais magufuli amekosa kuhudhuria mikitano mikuu miwili jijini Nairobi, iliyowaleta pamoja marais wengi wa Afrika.
Tangu aingie mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli ambaye ameamua kukabiliana na ufisadi nchini mwake amezuru tu Rwanda na Uganda.
Pia ziara ya Dkt Magufuli inahusia na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa muungano wa afrika-AU.
Tofauti na Tanzania, kashfa za mamilioni ya dola inafichuliwa mara kwa mara nchini Kenya, huku pesa za umma zikinyakuliwa na baadhi ya watu mashuhuri serikalini na walio na uhusiano wa karibu na watawala wa nchi hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta atamkaribisha mgeni wake jijini Nairobi, baada ya Kenyatta kukamilisha ziara ya siku mbili huko Khartoum, alipokutana na Rais wa Sudan- Omar Al- Bashir.
Ziara ya Magufuli nchini humo, inatukia wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegea.
Kwenye ajenda ya ziara hiyo rasmi ya kiserikali, kati yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili, kwani Rais magufuli amekosa kuhudhuria mikitano mikuu miwili jijini Nairobi, iliyowaleta pamoja marais wengi wa Afrika.
Tangu aingie mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli ambaye ameamua kukabiliana na ufisadi nchini mwake amezuru tu Rwanda na Uganda.
Pia ziara ya Dkt Magufuli inahusia na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa muungano wa afrika-AU.
Tofauti na Tanzania, kashfa za mamilioni ya dola inafichuliwa mara kwa mara nchini Kenya, huku pesa za umma zikinyakuliwa na baadhi ya watu mashuhuri serikalini na walio na uhusiano wa karibu na watawala wa nchi hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta atamkaribisha mgeni wake jijini Nairobi, baada ya Kenyatta kukamilisha ziara ya siku mbili huko Khartoum, alipokutana na Rais wa Sudan- Omar Al- Bashir.
TFDA yakamata dawa bandia zenye thamani ya shilingi milioni 17.4
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekamata dawa bandia aina tano katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini. Miongoni mwa dawa hizo ni dawa za Malaria.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii, jijini Dar es salaam,Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo,amesema mamlaka hiyo ilifanya utafiti katika kanda hizo baada ya kupata taarifa za uwepo wa dawa bandia kwenye maeneo ya mikoa ya Geita na Mara katika kipindi cha mwezi Agosti na Septemba mwaka huu.
“Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa dawa hizi bandia zinatengenezwa hapa nchini katika makazi ya watu na maeneo mengine ya kificho ambapo zilizoisha matumizi huongezewa muda kwa kuondolewa lebo za zamani na kuwekwa mpya,”amesema.
“Maduka 17 yaliyokutwa na dawa bandia na dawa za serikali yamefungwa, dawa zimekamatwa na pia inafungua majalada 38 katika vituo vya polisi dhidi ya watuhumiwa,” ameongeza.
Amesema TFDA imekamata dawa hizo bandia zenye thamani ya shilingi milioni 17.4 ambapo mkoa wa Mbeya umetajwa kuwa na idadi nyingi ya dawa hizo.
Aidha Sillo ametaja maeneo yaliyofanyiwa ukaguzi kuwa ni pamoja na famasi, maghala ya dawa, zahanati, maduka ya dawa za mifugo na muhimu na kwamba jumla ya maeneo 207 yalifanyiwa ukaguzi.
Mnamo Oktoba 4 hadi 6 2016 TFDA ilifanya operesheni maalumu ya ukaguzi kwa lengo la kubaini, kukamata, kuziondoa katika soko na kuwachukulia hatua za kisheria wanaojihusisha na biashara ya dawa bandia za serikali, zisizosajiliwa, pamoja na dawa duni na zile zilizoisha muda wake wa matumizi.
Picha: Show ya Diamond Malawi yafana licha ya mvua kubwa kunyesha
Licha ya mvua kubwa kunyesha, Diamond amefanikiwa kupiga show iliyofana kwenye Sand Music Festival iliyofanyika kwenye fukwe za Living stone Jumamosi hii.
Mpiga picha wake, Kifesi amedai kuwa mvua kubwa ilinyesha na kulazimu show yake kusimama kwa muda. Hata hivyo mashabiki waliokuwa na hamu kumuona akitumbuiza, walisubiri hadi ilipokata.
Kwenye show hiyo Diamond alitumbuiza live. Hizi ni picha zaidi: