Latest News
Loading...

Young Killer akaribisha watakaomsaidia kuandika mashairi

Young Killer amefungua milango kwa mwandishi yeyote anayeweza na mwenye nia ya kumwandikia wimbo utakaokuwa kwenye level zake.
Young Killer
Pia amekaribisha producer yeyote mchanga mwenye uwezo wa kutengeneza midundo mikali.
Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa huu ndio muda muafaka kwakuwa hakuwahi kuandikiwa nyimbo hapo kabla na mashabiki tayari wameshaufahamu uwezo wake mkubwa alionao kwenye sanaa.
“Nishaonyesha uwezo mkubwa na sikuwahi kuandikiwa nyimbo hata siku moja toka nimeanza,” amesema. “Sasa nafungua dirisha la usajili kwa yeyote anayetaka kuniandikia ngoma kali iwe na uwezo ambao mkubwa kama au zaidi na pia nakaribisha maproducer hata akiwa mchanga lakini ana uwezo ambao anaona utafanana na mimi namkaribisha,” amesisitiza.
Wiki hii rapper huyo aliachia ngoma mpya iitwayo Mtafutaji.

Miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta wakipata tabu na hata kufanya upasuaji hatari ili kuongeza makalio na wengi wameharibika kabisa au kupoteza maisha kwenye oparesheni hizo hatari. lakini kama jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo kitaalamu inaitwa gluteal maximus, gluteal minimus na gluteal medias.

Hiyo ndio misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi vizuri huongezeka na kua mikubwa. ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha mwili chenye misuli lakini sio kua makubwa tu lakini hata kuyafanya kua na shepu nzuri na kuvutia.. unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..

1. Mazoezi ya squat;
mazoezi haya huanzwa kwa kusimama na miguu yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka, mazoezi haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku za kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo zimeanza kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza makalio.fanya zoezi hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na tano au unaweza ukaanza kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja kisha ukaendelea na mazoezi ya kawaida kama nilivyoelekeza.
2. Zoezi la bridge;
watu wengi wanashinda wamekaa kwenye viti  mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata mtu mwenye makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno kwa juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa mbele kwa sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya hivi kwa kila mguu mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika mbili kila baada ya raundi.

3. Donkey kick;
piga magoti kisha weka mikono chini kama mbuzi anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu kisha rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na kuurudisha mara 20.

4. Kula protini nyingi:
vyakula vya protini ni muhimu kujenga misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa, karanga, korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.

5. Chagua aina nzuri ya wanga;
ulaji wa mikaango kama chips, chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta vitambi na kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.

6. Tumia mboga za majani; 
mboga za majani ni muhimu sana kwani husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na mwili kirahisi na kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.

 7. Tumia virutubisho vya kutosha;
virutubisho vyenye madini mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja kwa moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha wanaotumia virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia kabisa.jinsi ya kutumia; chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye virutubisho vyako kisha changanya na maziwa kwa upande wa protein shake na kwa upande wa argi changanya kijiko kimoja cha unga na maziwa ya mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku huku ukiendelea na mazoezi.

Mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua muda angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na haimaanishi kwamba ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana, mazoezi ni muhimu kwa mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la mwezi yaani mara moja kwa siku kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa wiki baada ya mwezi wa kwanza. kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi kufanikiwa, usije ukafanya zoezi siku mbili ukaacha afu ukategemea mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata virutubisho hivyo, kupata video za mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu zaidi.

Jinsi Mwanamke Anavyoweza Kuongeza Hips na Makalio kwa Vyakula na Mazoezi

Walichokusudia Kufanya Wanachama wa Yanga Leo Kuhusu Yusuph Manji Kuibwaga Yanga

Baada  ya taarifa za mfanyabiashara na mwenyekiti wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji kuripotiwa kukusudia kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya klabu ya Yanga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuandamwa na maneno na baadhi ya watu huku wana Yanga wengine wakiwa kimya.

Taarifa za Manji kujitoa zinakuja kwa sababu ya kudaiwa kujihisi mpweke kwani licha ya kushambuliwa kwa maneno na baadhi ya ya watu ikiwemo wanasiasa, hakuna mwanayanga aliyekuwa pamoja nae hivyo anajihisi mpweke na ana kusudia kujiweka pembeni.

Kufuatia taarifa za Manji kukusudia kujitoa viognozi wa Yanga wa kanda zote wamekusudia kufanya kikao leo saa 4 asubuhi makao makuu ya klabu hiyo kutoa tamko la pamoja kuhusianna maamuzi ya Manji, kujitoa kwa kuona anatengwa na wanachama.

Kundi la Original Comedy Matatani Kwa Kuvaa Sare za Jeshi la Polisi Kwenye Sherehe ya Masanja Mkandamizaji

katika  siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.

 Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.    

Picha: Tazama uzinduzi wa mashindano ya Olimpiki 2016 Brazil

Mashindano ya Olimpiki 2016 Ijumaa hii yalizinduliwa rasmi mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil na kupambwa na burudani ya tamaduni za nchi hiyo.
36EB96AF00000578-3726239-image-a-193_1470444704006
Pamoja na hivyo ufunguzi wa mashindano hao haukubarikiwa na raia wengi wa Brazil waliojikusanya nje ya uwanja kuandamana kuyapinga.
Wananchi hao walipambana na polisi waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha. Ndani ya uwanja huo wa Maracana wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 kulikuwa na viti vitupu kibao. Tazama picha mbalimbali za ufunguzi huo.

36EA4EE500000578-3726239-image-a-26_1470437762551

36EB6E2100000578-3726239-image-a-133_1470441937041

36EB9D0300000578-3726239-image-a-217_1470445477840

36EBA62000000578-3726239-image-a-247_1470447087755

36EBBCCA00000578-3726239-image-a-280_1470449502306

36EBEBE800000578-3726239-image-a-39_1470459539188

36EC2DB400000578-3726239-image-a-294_1470450133016

36EC4A7900000578-3726239-image-a-30_1470456617317

36EC6BBA00000578-3726239-image-a-364_1470455162765

36EC7A5B00000578-3726239-image-a-352_1470455071137

36EC7E9F00000578-3726239-image-a-354_1470455073743

36EC16CD00000578-3726239-image-a-270_1470448870038

36EC71CD00000578-3726239-image-a-359_1470455095301

36EC147D00000578-3726239-image-a-267_1470448859222

36EC286A00000578-3726239-image-a-286_1470449963479

36EC596D00000578-3726239-image-a-346_1470454919880

36EC355000000578-3726239-image-a-3_1470455993609

36EC567500000578-3726239-image-a-337_1470453823628

36EC574900000578-3726239-image-a-351_1470455061750
36ECE7D900000578-3726239-image-a-15_1470472498894

Video: Hans J – Jiandae

Video mpya ya msanii Hans J wimbo unaitwa “Jiandae”, Video imeongozwa na Khalfani.

Music: Christian Bella – Nishike

Mfalme wa masauti Christian Bella baada ya kuachia video ya wimbo “Nishike”, Hii ni Audio ya wimbo huo. Producer Abby Dad.

Video: Britney Spears ft. G-Eazy – Make Me

Britney Spears is looking for a leading man to cast in her new video for “Make Me…” featuring G-Eazy.

Video;Itazame Historia Zari The Boss Lady Pamoja na Utajili Wake.

Je unamjua Vizuri Zari Hassan Mama Mtoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz?
Video hii Hapa chini itakupa kujua Zari ni Nani pamoja na thamani ya utajiri wake
Tazama Video:

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda Apiga Marufuku Maandamano ya UKUTA, Awapa Rungu FFU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwepo kitu kinaitwa UKUTA ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

Akizungumza na kikosi cha kutuliza ghasia katika kambi ya Ukonga Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa askari wanafahamu sheria wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo au maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshaagiza kinachotakiwa ni utekelezaji.

‘’Msisubiri maelekezo yoyote kutoka juu, asiwepo mtu yeyote atafunga duka kwa sababu ya UKUTA nyie ni matrekta hakuna UKUTA unaweza kusimama mbele yenu, mimi kama Mkuu wa Mkoa ninaamini hatutakuwa na vurugu kwenye Mkoa wetu na hatuwezi kuruhusu vurugu kwa kuwa tunajua madhara ya vurugu’’ Amesema Makonda.

Aidha kwa upande wake Kamanda wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema jeshi la polisi lipo vizuri na vijana wameandaliwa vizuri na wameandaliwa kuwa tayari siku nyingi na hakuna mtu yeyote atakayethubutu kufanya UKUTA na watakaofanya hivyo watazimwa kabla hawajafanya chochote.

Kamada amewataka wananchi wote Jijini Dar es Salaam kuto jitokeza kwenye oparesheni UKUTA kwa kuwa maandamano hayo siyo halali na watakaojitokeza watapata matatizo yasiyowahusu.

Oparesheni UKUTA ilitangazwa na CHADEMA ikiwa na maana Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania na ikatajwa tarehe Mosi Septemba nchi nzima chama hicho kitafanya mikutano ya hadhara jambo ambalo limepingwa na serikali kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufuatia wakuu wa mikoa.

Salam za Wema Sepetu kwa mtoto wa Diamond Platnumz ‘Tiffah’

Msanii wa filamu Wema Sepetu anaendelea kuuthibitishia umma kwamba hana tena kinyongo na Ex wake wa zamani Diamond Platnumz baada ya Jumamosi hii kumwandikia ujumbe mzuri bintiye Diamond, Tiffah katika siku yake ya kuzaliwa.

Wawili hao hivi karibuni wameonyesha kushirikiana mambo kadhaa katika mitandao ya kijamii licha ya wiki mbili zilizopita kusambaa kwa tetesi ya kurudiana na baadae kukanushwa na Wema Sepetu.

Muigizaji huyo kupitia instagram ameandika ujumbe huu:

Happy Birthday Princess Tee…🎈🎉🎁🎊🎀💝 May Allah bless your precious lil self… You will definitely turn out to be a phenomenal young woman… Princess_tiffah.

Jumamosi hii bintiye Diamond, Tiffah, ametimiza mwaka mmoja ambapo amewashukuru wote waliomtakia heri katika siku hiyo.

“Today a year ago at 4:40 am in the wee hours of the morning I was brought into this world. Thank-you for all my bday wishes & God bless all of you😘. HAPPY BIRTHDAY TO ME,” Ujumbe huu uliandikwa instagram ya binti huyo.

Mgeja Atoa yamoyoni Juu ya Rais Magufuli

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema hatua ya Rais John Magufuli kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini, imelenga kuminya demokrasia na serikali kutaka kutokosolewa.

Mgeja, ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo haikubaliki katika nchi ya kidemokrasia duniani kwa kuwa uhai wa vyama vya siasa upo katika mikutano.

Pia amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kushughulikia migogoro ya vyama badala ya kusubiri hadi nchi ikielekea katika mgogoro mkubwa.

Alisema kauli ya Rais Magufuli kwamba shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020, inakiuka katiba kwa kuwa mikutano na shughuli za vyama vya siasa vipo kikatiba.

Alieleza kuwa kinachotokea sasa kwa viongozi wa upinzani ni kupigania demokrasia hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Serikali inakosolewa kupitia mikutano ya vyama vya siasa na serikali isitupangie cha kuzungumza. Kutokana na kauli ya rais tunaonya likitokea lolote katika mikutano ambayo itafanyika nchi nzima, kupitia operesheni ya Umoja wa Kuondoa Udikteta Tanzania (Ukuta), Rais atawajibika iwapo nguvu ya jeshi polisi itatumika,” alisema.

Msajili wa vyama vya siasa nchini atoa ya moyoni juu ya CHADEMA

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu mikutano ya hadhara na maandamano yanayotarajia kuanza Septemba 1 mwaka huu.
DSC_1495-620x312
Alhamis hii, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe alitangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi kwa dharura huku kufanyika kwa mikutano ya hadhara na maandamano kote nchini kuanzia Septemba 1.
Mbowe aliwataka viongozi wa Chadema katika ngazi zote hapa nchini, wabunge na madiwani kufanya maandalizi ya mikutano na maandamano huku pia akitangaza kuanzishwa kwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA).
Hata hivyo, Jaji Mtungi mapema hii leo amevieleza vyombo vya habari kuwa, “tamko la Chadema limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, linaloudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani.”
Pia amewaeleza kuwa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 katika kifungu cha 9 (2) (c) inakataza chama chochote cha siasa hapa nchini kutumia na kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake kisiasa.
“Si hayo tu, bali pia kifungu cha 9 (2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambao unaweza kusababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani,” amesema Jaji Mutungi.
Mvutano baina ya Chadema na jeshi la polisi juu ya kufanyika kwa mikutano ya hadhara umekuwa ukiendelea kwa muda sasa, kufuatia jeshi hilo kutoa tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara Juni mwaka huu kwa madai ya kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Kijana mbaroni kwa kumtukana Rais Magufuli hadharani

Mgomo wa daladala Jijini Mwanza umesababisha kijana mmoja Jijini humo kutamka lugha chafu ndani ya gari ambayo alipewa lifti limemsababishia kuishia mikononi kwa sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast dereva wa wa gari likitoa lifti Hassan Bushagama mkazi wa Buhongwa Jijini Mwanza asema alipofika eneo la Buhongwa akiwa na usafiri wake aina ya Toyota Noah kutokana mgomo wa daladala aliamua kutoa lifti kwa abiria aliowakuta hapo.

"Walipanda watu kama nane ambapo Dada mmoja akasema watu walivyo hawatakawia kusema Rais Magufuli ndiye anatakiwa aulizwe,kijana mmoja wa umri wa miaka kama 27 au 28 hivi akadakia akasema Rais ni '******** 'mzee mmoja akamwambia kijana tengua kauli lakini akakataa na kusisitiza ,abiria wakataka kumpiga nikawaambia mwacheni tumpeleke 'polisi " Amesema Bwana Bushagama.

Bushagama ameendelea kusema kwamba "Baada ya hapo niliendesha gari langu hadi kituo cha polisi tulipofika pale nikawaambia polisi hali halisi askari akawahoji abiria wakaelezea hali hiyo na yeye alipoulizwa akasema ,amesema hivyo lakini hakujua kama ingepelekea kufika huko.

Aidha Bushagama ameongeza kuwa wameamua kusitisha kazi zao na kuonesha uzalendo ili kuonesha kwamba Rais hawezi kutukanwa namna hiyo.

Kwa upande wake Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwama kijana huyo amejitetea na kusema kwamba alisema alimaanisha wanaogoma wanajifanya wapumbavu lakini Rais ni ******** zaidi yao jambo liliwakasirisha wenzake na kuamua kumfikisha kituo cha Polisi.

Kamanda ameongeza kuwa suala hilo tayari limefikishwa Polisi kitachoendelea ni ushahidi ukitosheleza kijana huyo atapelekwa mahakamani.

Hatimaye Msanii Ney wa mitego kasalimu amri

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego ameanza kutekeleza baadhi ya maagizo aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’.
Rapper huyo alipewa adhabu hiyo pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni 1 baada ya kukutwa na makosa matatu likiwena la kutojisajiri katika baraza hilo.
Katika taarifa aliyotoa Nay wa Mitego, ameonyesha kujuta huku akiwaomba radhi mashabiki wa muziki wake kama ambavyo aliagizwa na BASATA.
“Wakati naandika wimbo “Pale Kati” nilikua nimeangalia nyimbo zilizowahi kutoka nyuma na zilizoko sokoni sasa, sikuona kama mistari yake ina matatizo. Lakini baada ya kukaa pamoja na kusikiliza mstari kwa mstari tumegundua kwamba kuna baadhi ya mistari ilikua ina maneno makali. Hivyo basi naomba radhi kwa mtu yeyote alieumizwa au kukwaza na mistari hiyo. Tusikilizie kifuatacho.!! “Pale kati” jamani,” aliandika Nay wa Mitego kupitia instagram yake.
Pia rapper huyo ametakiwa kujisajiri katika baraza hilo pamoja na kuachana na kuimba vyimbo ambazo zinawazalilisha akina dada.