Latest News
Loading...

Wastara apata shavu la ubalozi wa kampuni mpya ya simu, atavuna Tsh milioni 400 kwa miaka 2

Malkia wa filamu Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa kampuni ya simu za mkononi ya KZG Tanzania yenye makao makuu yake nchini China.
?
Wastara akionyesha mkataba
Katika mkataba huo mwigizaji huyo atavuna kiasi cha tsh milioni 400 kwa miaka miwili akiwa balozi wa kampuni hiyo kwa matangazo na matamasha mbalimbali.
Akiongea na Filamu Central meneja mauzo wa kampuni ya KZG Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa kamapuni yao imelenga kusambaza teknolojia vyuoni kwani wana bidhaa nyingi ambazo zinatumika katika kufundishia wanafunzi hao.
“Leo pia tunazindua simu ya kipekee kabisa kufika hapa nchini Kzg Kimi ambayo inatumia betri ya ndani kwa ndani ambayo ina sifa ya kutengenezeka tofauti na zingine ambazo betri zake zikiharibika hazitengenezeki,”alisema Kalikawe.
Pia Wastara ameishukru kampuni hiyo kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zilizalishwazo na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Computer na vifaa vingine vya teknolojia.
Uzinduzi huo ulisindikizwa na wasanii wa Bongo movie wakimpongeza Wastara kuingia mkataba huo.

Tibaijuka agoma kuchukua milioni 200 za tuzo

Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ametunukiwa tuzo ya heshima ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalfa bin Salman Al Khalifa ikiwa ni utambuzi wa mchango wake wa kuchochea maendeleo
dntibaijuka1110a
Tibaijuka ameyasema jana wakati akizungumza na wanahabari kwa lengo la kuelezea namna alivyopatiwa tuzo hiyo pamoja na fedha kiasi cha dola laki moja ambayo amekataa kuichukua kutokana na hofu ya kukumbwa na kashfa kama ile iliyomkumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne.
Pia alisema kuwa tuzo hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Bahrain na hutolewa baada ya miaka miwili kwa mtu ambaye ametoa mchango mkubwa katika kutatua changamoto za sekta mbalimbali za kiuchumi ambazo zinawakumba wananchi.
Profesa Tibaijuka alifafanua kuwa tuzo hiyo imetokana na kushughulikia malengo ya milenia wakati akiwa anafanya kazi katika Umoja wa Mataifa (UN) na kusema kuwa tuzo hiyo ni heshima kwa watanzania kwani alienda kuwawakilisha kwenye umoja huo.

Ushindi wa Genk ya Samatta uliowafanya waongoze Kundi F Europa League


Usiku wa Septemba 29 2016 klabu ya KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa Kundi F wa Europa League dhidi ya Sassuolo ya ItaliaGenk waliwakaribisha  Sassuolo katika uwanja wao wa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rapid Wien.
Katika mchezo huo ambao KRC Genk waliingia kwa dhamira moja tu ya kupata point tatu, ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 8, mjamaica Leon Bailey dakika ya 25 naThomas Buffel dakika ya 61 wakati Sassuolo waliishia goli moja lililofungwa na Matteo Politano dakika ya 65.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alikuwa majeruhi aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya mgiriki Nikolaos Karelis aliyekuwa kwafunga goli la kwanza la Genk, ushindi huo wa KRC Genk unakuja ikiwa ni baada ya kukubali kipigo cha goli 3-2 katika mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Rapid Wien, Genk sasa watacheza mchezo wao wa tatu October 20 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania.

Hatimae Man United wapata ushindi wa kwanza Europa League


Baada ya kuanza vibaya kwa klabu ya Man United katika mchezo wake wa kwanza waEuropa League dhidi ya Feyenoord nchini Uholanzi, usiku wa Septemba 29 Man Unitedwalishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi A Europa League dhidi yaZorya.
38eee44600000578-3814356-image-a-90_1475181520619
Man United ambao mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Feyenoordambao walikuwa na rekodi ya kushinda mechi nane mfululizo, wamecheza mchezo wao wa pili wa Europa League dhidi ya Zorya katika uwanja wao wa Old Trafford na kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 69.
38eee11f00000578-3814356-image-a-87_1475181251503
Kufuatia ushindi huo  Man United wanakuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Fenerbahce aliyepata ushindi wa kwanza wa Europa League leo dhidi ya Feyenoord na kuivunjia rekodi yao ya kucheza mechi 9 bila kufungwa, nafasi ya pili wakiwa Feyenoord na Zorya wakishika mkia kwa kusalia na point moja, Man Unitedwatacheza mchezo wao wa tatu dhidi ya Fenerbahce October 20 2016.

38ef2a3700000578-3814356-image-a-21_1475183714544

Magazeti ya Tanzania September 30, 2016


20160930_041527

20160930_041549

20160930_041603

20160930_041612

20160930_041624

20160930_041631

20160930_041639

20160930_041646

20160930_041706

20160930_041714

20160930_041723

20160930_041730

20160930_041738

20160930_041744

20160930_041752

20160930_041758

20160930_041806

20160930_041814

20160930_041823

20160930_041828

20160930_041836

20160930_041843

20160930_041851

20160930_041857

20160930_041907

20160930_041914

20160930_041922

20160930_041927

20160930_041946
20160930_041954

Manji aizawadiwa Yanga ekari 715 zijengwe uwanja wa kisasa maeneo ya Kigamboni

Hatimaye klabu ya Yanga imepata sehemu nyingine ya kujenga Uwanja wa kisasa kutoka kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yussuf Manji ametoa eneo la ekari 715 na kuikabidhi klabu hiyo maeneo ya Kigamboni Geza Ulole jijini Dar es Salaam maalum kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na wa klabu hiyo.
img-20160928-wa0045
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Mambi ya Ndani, Mwigulu Nchemba, mke wa rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Sheikh Abeid Amaan Karume, Mama Fatma Karume ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, ndiye aliyepokea eneo hilo.
img-20160928-wa0039
img-20160928-wa0041
yanga-na-manji-559x520
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mama Karume amesema wao kama Baraza la Wadhamini wanashukuru sana kupokea eneo hilo, kwani wanaamini ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wao walipoketi kujdili suala hilo hatimaye imetimizwa.
Yanga wamepata eneo hilo huku mahasimu wao Simba wakiwa katika hatua za ujenzi wa uwanja wao uliopo Bunju.

Yemi Alade akiishi alichokifanya Michael Jackson, Brazil

Staa wa Nigeria, Yemi Alade ametumia location iliyopo nchni Brazil kwenye mji wa Rio de Jeneiro ya Favela of Dona Marta aliyowahi kuitumia mfalme wa muziki wa pop duniani, marehemu Michael Jackson kwenye video ya wimbo wake wa ‘The Don’t Care About Us.’
yemi-alade-brazil-10-600x400
Yemi yupo nchini humo kwaajili ya mradi wa kampuni ya mafuta ya Shell, uliopewa jina ‘Make The Future’ akiungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Jennifer Hudson, Pixie Lott, Steve Aoki, Tan Wei Wei na Luan Santana.
yemi-696x661
yemi-alade-brazil-4-600x400
yemi-alade-brazil-5-600x900
yemi-alade-brazil-12-600x400
yemi-alade-brazil-13-600x400
yemi-alade-brazil-1-600x400
yemi-alade-brazil-2-600x400
yemi-alade-brazil-3-600x400
Hata hivyo Michael Jackson alikutana na wakati mgumu kutoka kwa serikali ya Brazil kutokana na kuzuiwa kushoot video yake kwenye eneo hilo kwakuwa kipindi hicho mji wa Rio haukuwa mkubwa na waliamini hautaitangaza nchi yao vizuri.
yemi-alade-brazil-6-600x400