Latest News
Loading...

Salamu ya Maalim Seif yabamba Mitandaoni Nchini


 Picha inayomuonyesha Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa ameinama mikono ikiwa tumboni, huku Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akiwa amenyoosha mkono kuashiria kutaka kusalimiana na katibu huyo mkuu wa CUF, sasa imekuwa moto mtandaoni.

Picha hiyo ilichukuliwa wakati wa shughuli za mazishi ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi kisiwani humo mapema wiki hii, na sasa inaigizwa na watu wa kariba tofauti wanaotuma mitandaoni picha inayofanana na tukio hilo.

Picha hizo zinaonyesha watoto, vijana na hata watu wa makamo wakiigiza tukio hilo.

Wawili hao walipambana kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar uliofutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais. CUF ilisusia uchaguzi mpya uliotangazwa na Jecha.

Vitendo hivyo vya kuigiza matukio ya watu muhimu sasa vimepamba moto mitandaoni. Miongoni mwa matukio yaliyoigwa sana mitandaoni ni la waziri wa zamani wa kilimo, Steven Wasira kupiga picha akiwa hajafunga vizuri vifungo vya koti na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kudondoka.

Pia tukio jingine lililoigwa sana ni la Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuonekana amekaa kwenye kiti pembeni ya barabara akiongea na simu huku msafara wake ukiwa unamsubiri.

Masanja asema Orijino Komedi imemalizana na polisi, ni issue ya kuvaa sare za polisi


Baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwakamata baadhi ya wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kosa la kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Masanja Mkandamizaji amedai tayari wameshamalizana na jeshi hilo baada ya kuomba msamaha.

Mchekeshaji huyo ambaye kwa sasa yupo honey moon visiwani Zanzibar, amesema ameamua kutoa taarifa hiyo ili kuwaondoa hofu baadhi ya mashabiki pamoja na ndugu.

“Jamani asanteni kwa maombi na meseji zenu kuulizia juu ya inshu ya polisi, tunamshukuru mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha,” aliandika Masanja facebook.

Aliongeza, “Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini akina Joti, Seki, Maclegan,na Wakuvanga wamepata kautamu kidogo kamahojiano. Na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu,”

Wasanii hao walikamatwa na jeshi la polisi na kuhojiwa baada ya kuvaa sare zinazofanana ya za jeshi la polisi katika harusi ya msanii mwenzao Masanja Mkanadamizaji.

Olimpiki: Mwanariadha wa Kenya Apokonywa Medali Kwa Kosa la Udanganyifu


Mwanariadha kutoka nchini Kenya aliyeshinda medali ya shaba kwenye riadha na kuruka vihunzi pamoja na maji, Ezekiel Kemboi amepokonywa medali yake kwa kosa la udanganyifu mchezoni kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea huko nchini Brazil.

Kemboi (34) alimaliza kwenye nafasi ya tatu ya mashindano hayo ya kukimbia ya mita 3000 kwa kutumia muda wa 8:08.47. Ufaransa ilipinga ushindi huo wa Kemboi kwa kukata rufaa baada ya kubainika kuwa mwanariadha huyo wakati akiendelea na mbio hizo baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari.

Kamati ya mashindano hayo imekubali rufaa hiyo na kuamuru kumpatia medali hiyo ya shaba, Mahiedine Mekhissi kutoka Ufaransa aliyeshika nafasi ya nne baada ya kukimbia kwa muda wa 8:11.52.

Hata hivyo Kemboi ambaye alikuwa bingwa wa mbio hizo kwenye mashindano ya Olimpiki ya 2012 ya nchini Uingereza amedaiwa kutangaza kustaafu kucheza mchezo huo.

Fid Q: Mapenzi Yamenitesa Sana Jamani!

AGOSTI 13, mwaka huu ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwanahip Hop, Fid Q na kwa furaha aliyonayo kwa kutimiza miaka kadhaa, siku hiyo aliamua kuachia ngoma mbili kama zawadi kwa mashabiki wake.
Fid-q
Wimbo wa kwanza unaoitwa Sumu aliutoa usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, baadaye jioni akaachia video ya ngoma nyingine ya Roho aliyomshirikisha Christian Bella.
Licha ya uzuri wa video na ujumbe, lakini Fid Q ambaye jina lake halisi ni Fareed Kubanda anakiri wimbo wa Roho umegusa kisa cha kweli cha mapenzi kilichomtokea miaka iliyopita na ndiyo maana anaonekana na kusikika akiimba akiwa na hisia kali.
“Mapenzi ni matamu, nahofia kuumizwa moyo, nashindwa kujaribu roho inaniuma sana, roho inaniuma roho inaumaaa…’’
Hiyo ni sehemu ya mashairi ya Bella katika wimbo huo. Fid Q naye kuna sehemu anaimba:
“Haki ya Mungu tena chuki humchoma anayeihifadhi, kumsahau sana siwezi… mapenzi yalifanya nikaumbuka ninachoshukuru hayakuniua.”
Championi Ijumaa limezungumza na Fid ikiwemo uamuzi wa kwenda kutengeneza video ya Roho nchini Sweden:
“Ingawa ni muda mrefu sana tangu nilipokutwa na mkasa huo wa kimapenzi lakini nimeamua ‘ku-share’ na jamii katika kipindi hiki. Nimeamua hivyo kwa kuwa kilichotokea nimeshasamehe na nimeanza kusahau,” anasema Fid kisha mahojiano yanaendelea:
Beat ya Roho ilitumika katika wimbo wa Haki mwaka 2014, imekuwaje umesikika tena kwako?
“Ni kweli, tena ilitumiwa na wasanii wengi wa Hip Hop katika ule wimbo ambao January Makamba naye alifanya ‘intro’. Kilichotokea ni hivi, tayari nilikuwa nimeshaitumia hiyo beat katika wimbo huohuo wa Roho ila nilikuwa sijautoa.
“Sasa ilipokuja ishu ya kuimba Haki, P-Funk akahitaji kuitumia beat hiyohiyo. Kwa kuwa ‘idea’ za ujumbe zilikuwa tofauti nikaona siyo mbaya, kwa hiyo akaibadili kidogo, tukafanya ngoma na hakuna tatizo lolote.
Ilikuwaje ukamshirikisha Bella?
“Nilihitaji kufanya kitu cha tofauti tu ambacho nahisi nimefanikiwa. Haikuwa shida kumpata Bella, nilipomshtua akakubali maana ni shabiki wa ngoma zangu pia, nashukuru alinipa ushirikiano mkubwa kukamilisha hii kitu ndiyo maana hata mimi nilipomuandikia script (mwongozo) ya video yake ya Nishike nilifanya kwa roho moja.
Script ya Roho nani aliandika?
“Niliandika mimi lakini nilipoenda Sweden madairekta wakairekebisha kidogo kwa kuwa wao ndiyo wanafahamu zaidi mazingira na mitaa ya Sweden kuliko mimi. Sababu ya kwenda huko ni kubadili upepo na kuwa na kitu cha tofauti.
Kuna sehemu umevaa ‘hood’ (nguo nzito) inaone-kana kama imeanza kuchoka na kuchanika, ilikuwaje?
“Ile ni staili tu kama ilivyo kwa Kanye West anavyovaa zile nguo kama za watu wa zamani. Hii staili niliyoifanya inaitwa Rough, Rugged & Raw, ni ishu ya kuwakilisha zaidi kitaa ila naona kama imekuwa gumzo hivi, hivyo naweza kuanzisha nguo zangu za dizaini hiyo.
Tofauti na Bella kuna sauti inasikika, ni nani huyo?
“Yule anaitwa Paul Ndunguru, anatoka Wa Hapahapa Band, ni mchoraji mzuri, anaandaa vitabu na anapinga ukatili wa mauaji ya tembo, naye haikuwa shida kumpata, nikafanya naye kazi vizuri tu.
Gharama nzima ya video ni kiasi gani?
“Mzoefu anaweza kukisia ni kiasi gani kwa maana ya nauli ya kwenda kule, kugharamia mamodo na kila kitu, japokuwa naona kimsingi tuangalie zaidi ubora wa kazi iliyotoka kuliko gharama, maana hata nchi za wenzetu hawazingatii sana gharama zaidi ya kazi iliyofanyika.
Vipi kuhusu video ya Sumu?
“Video ya Sumu ndiyo ipo kwenye maandalizi, Roho itaangaliwa na Sumu itaendelea kusikilizwa kwenye redio kwa kuwa hata meseji ni mbili tofauti.”
Vipi kuhusu kolabo za kimataifa?
“Hizo zipo lakini siwezi kuongeza chochote hapo kwa kuwa mwenye mamlaka ya kuzungumzia hizo ishu ni Cheusi Dawa, maana ndiyo wasimamizi wa kazi zangu.”
Chanzo:GPL

VIDEO: Ajali ya gari ndogo na lori iliyotokea kati ya mataa ya Mlimani City na TCRA


Usiku wa August 19 maeneo ya mataa yaliyopo kati ya Mlimani City na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitokea ajali ya gari ndogo ambayo haikuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kugongwa na Lori lililovuka na kuingia hadi kituo cha mafuta kilichopo jirani na mataa hayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo gari ndogo ilikuwa  ikiendeshwa na mwanamke ambaye mwili wake haukuwa umeweza kuokolewa kutokana na kubanwa.
.

Lady Gaga apata shavu kwenye filamu mpya ya ‘A Star Is Born’

Msanii wa muziki wa Pop Marekani, Lady Gaga amepata shavu la kuigiza kwenye filamu mpya ya ‘A Star Is Born’ akiwa kama mmoja wa mastaa kwenye filamu hiyo.
Lady Gaga
Hii itakuwa ni toleo jipya la filamu hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1954 lakini hapo awali nafasi hiyo ilipangwa kuchukuliwa na Beyonce. Mwigizaji Bradley Cooper anatajwa kuwa muongozaji huku Billy Gerber na Jon Peter wakiwa ndio watayarishaji wa filamu hiyo.
Mbali na kuigiza lakini pia Lady Gaga anatarajiwa kuandika na kuimba nyimbo mpya kwa ajili ya filamu hiyo. Filamu hiyo inatarajiwa kuanza kuchezwa kuanzia mwakani.
Lady Gaga anaungana na wasanii wengine wa Marekani waliopata shavu la kuigiza kwenye filamu tofauti akiwemo Mariah Carey, Rihanna na wengine wengi.

Snoop Dogg ampa shavu Nay wa Mitego (Video)

Baadhi ya wana hip hop wanadai kuwa Nay wa Mitego hafanyi hip hop halisi, lakini rapper huyo controversial amepata shavu ambalo hakuna msanii wa hip hop Bongo amewahi kulipata – kupewa shavu na rapper mkongwe, Snoop Dogg.
snoop-dogg-4ddc3edb2d557
Asante kwa video ya kuchekesha inayomuonesha babu akicheza na mwanamke mwenye makalio ya haja iliyochanganywa na sauti ya wimbo wa mpya wa Nay wa Mitego, Good Time, sauti yake imesikika kwa followers kibao wa Snoop Dogg.
Haijulikani ameipata wapi video hiyo, lakini Snoop ameipost kwenye akaunti yake ya Instagram yenye followers zaidi ya milioni 11.8.

Kidogo ya Diamond yapanda daraja BBC Radio 1Xtra

Diamond Platnumz anachekelea tu sasa hivi kwasababu wimbo wake Kidogo aliowashirikisha mapacha wa P-Square umepanda daraja zaidi kwenye playlist za redio yenye heshima kubwa Uingereza, BBC Radio 1Xtra.
14052731_611870808981058_626144385_n
Na ili kujua ukubwa wa hiki kilichotokea ni vyema ukafahamu kuwa ni nyimbo chache sana za Afrika zilizowahi kuingia kwenye playlist ya kituo hicho maarufu kwa burudani UK.
Tuliripoti siku chache zilizopita kuwa wimbo wake huo umeingia rasmi kwenye playlist zake lakini ukawa umewekwa kwenye orodha C. Na sasa wimbo huo umepanda hadi orodha B.
13725769_1656215124706526_685639101_n
Diamond hajaficha furaha yake kufuatia kupanda daraja kwa wimbo wake huo.
“Dear God i wanna thank you, for everything 🙏…. #KIDOGO on the BBC Radio 1xtra PlayList from C list last week to B list this week…. thanks alot BBC Radio 1xtra and my all UK fans for the Big Support,” ameandika kwenye Instagram.
Iwapo wimbo huo utapanda hadi orodha A, maanake ni kuwa utakuwa kwenye rotation kubwa zaidi kwa siku huku pia akipokea mrabaha mkubwa kutokana na kuchezwa ngoma yake – wenzetu hawachezi ngoma za wasanii bure etii!

Kama Umesoma au Unasoma Kwa Lengo la Kuja Kupata Pesa; Unaweza Kuja Kujidharau na Kuwa 'Disappointed'


Kama umesoma[au unasoma], kwa lengo la kuja kupata pesa; unaweza kuja kujidharau na kuwa "disappointed". Kwa sababu huku mtaani kuna watu ni ama la saba au hata la saba hawakumaliza lakini ndio wanaoongoza kumiliki pesa za kutisha. Ukipata nafasi ya kusoma; soma kwa bidii, lakini ni vema ukatambua kuwa [fedha za maana] ni nadra sana kukaa kwenye vyeti. Vyeti vikijitahidi sana vitaishia kukupa pesa ya kubadilishia mboga. Akili inayokupa vyeti madarasani ni tofauti kabisa na akili inayotumika mtaani katika utafutaji wa pesa! ‪#‎SmartMind

Wema Sepetu na Petit Man Wamaliza Tofauti zao


Kwa miezi kadhaa sasa Wema Sepetu na Petit Man walikuwa wakichuniana hadi kuwafanya mashabiki waanze kuuliza maswali kupitia mitandao ya kijamii kutaka kujua kunani!

Lakini usiku wa August 16, wawili hao walionekana wakijirekodi video fupi na Wema akaiweka katika account yake ya SnapChat. Baadaye kulivyokucha Wema alionekana kupost video clip ile ile ya SnapChat kwenye Instagram kuandika hivi: Yes…! He has a piece of me… @officialpetitman_wakuachetz”

“Mimi sidhani kama nina tatizo na Wema. Ndiye aliyenifanya mimi nijulikane na Wema ndiye mtu ambaye mimi nimetoka naye mbali sana miaka tisa. Kwahiyo hata kama nikiwa nimegombana naye siwezi nikasema siongei naye, kwahiyo mimi nahesabia sina tatizo naye kama watu wanavyodhani,” alisema.

Dereva Taxi Jela Maisha Kwa Kulawiti Mtoto Ndani ya Gari


Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu kifungo cha maisha jela, dereva taksi Ally Mzako (29) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka mitano.

Mzako ambaye ni mkazi wa Kinondoni, anadaiwa kumbaka mtoto huyo ndani ya gari, wakati mama wa mtoto huyo alipomuacha katika gari hiyo na kwenda duka la kubadilishia fedha za kigeni.

Hakimu mkazi, Flora Haule amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi wa mashahidi sita wa  upande wa mashtaka dhidi ya mshtakiwa.

Mzako alifanya kosa hilo, Julai 19, 2014, eneo la Clock Tower, mtaa wa Samora.

Jibu la Mwimbaji Emmanuel Mbasha Kuhusu Kurudiana na Flora Mbasha


Kama utakuwa unakumbuka mnamo September 21,2015 moja ya stori kubwa iliyogusa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ni ishu ya Hukumu ya Kesi ya Mwimbaji wa Gospel Tanzania, Emmanuel Mbasha ambapo alikuwa anakabiliwa na Kesi ya kumbaka shemeji yake na kesi imekuwa Mahakamani tangu 2014.

Wengi tunafahamu kwamba mwimbaji huyo aliachiwa huru baada ya Mahakama kumkuta hana hatia kwenye Kesi hiyo, sasa leo kajibu swali kuhusu kurudiana na mkewe Flora Mbasha na kuyaongea haya:

‘Mimi kurudiana na Flora Mbasha ni ngumu kwasababu yeye ndio aliniacha mimi na yeye ndio aliandaa mazingira yake ya kuniacha mimi mpaka ikafika wakati Familia yangu, viongozi mbalimbali wa Dini wakawa wanamshauri lakini akutaka kurudiana na mimi kwahiyo naweza sema ni ngumu kurudiana na Flora

Wizkid Asema Kidogo ya Diamond Ndio Nyimbo Bora na Anayoikubali Kwa Sasa


Msanii mkali wa africa na dunia kutoka nigeria wizkid akiongea na clouds fm amesema kwa sasa nyimbo ya diamond platnumz aliowashilikisha psquare kidogo ndio nyimbo bora kwake na ndio anayoukubali.

Wizkid pia hakusita kumpongeza diamond platnumz baada ya nyimbo hiyo kuingia kwenye chat za BBC 1xtra UK na kupata rotation.

Katika chat hiyo ni wasanii 2 tu kutoka africa walioingiza nyimbo zao , kidogo ya diamond na shabba ya wizkid mwenyewe akiwa na chriss brown, french montana na trey songz.
Wizkid jumamosi hii atakuwa Tanzania jijini mwanza kutumbuiza kwenye show ya fiesta

Picha za Masanja na Mke wake Zazua Maswali Kwa Mashabiki wake..Wadai Mke wa Mchungaji Apaswi Kuvaa Hivyo


Baada ya Harusi ya Mchekeshaji Masanja na Mkewe iliyofungwa Jumapili iliyopita wawili hao wameonekana kwenye picha mbali mbali wakijivinjari Honey Moon huku mavazi yao yakileta mabishano kama kweli ni Baba Mchungaji na Mama Mchungaji....

Baadhi ya Comments kwenye picha hizo hizi Hapa:

"Wachungaji wa mwendo kasi.."

"Kwa jinsi walivyovaa Biblia Takatifu inatufundisha kuwa utaweza kuwatambua kama ni nkweli wachungaji wa Kanisa la Mungu au watumishi wa kitapeli. Hivi vitu havijifichi. Mtumishi wa Mungu haachi maswali na hata akijifanya kwamba hamfahamu Mungu atajulikana tu kuwa ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Petro alipojaribu kusema hamfahamu Yesu na akaanza kuondoka ila waliokuwepo wakasema kuwa hata anavyotembea inadhihirisha yeye ni mtu wa Kristo. Je kwa muonekano wa Masanja, yeye ni mtumishi wa Mungu aliye hai????"


"Don't judge by looks....THE LORD GOD ALMIGHTY knows the hearts of everyone"


"Mavazi yanaonyesha uhalisia wa mtu. Kuna mavazi ambayo KAMWE mtu wa Mungu hawezi kuyavaa au kumruhusu mtu anayemmiliki kuvaa. Ila sijayaongelea mavazi aliyovaa Masanja"

"The Bible teaches us how to distinguish false from true prophets. Follow the Bible!!!"

"Dah!Mke wa masanja ana ugonjwa wangu kwa kweli"

Na wewe toa Maoni yako:

HATARI:Waliotafuna Fedha za Mikopo Wapewa Siku Saba Kuzirejesha


Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu (HELSB)na wa vyuo vilivyohusika kufanikisha malipo ya fedha za mikopo kwa wanafunzi hewa kuchukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kurudisha fedha zilizochukuliwa na wanafunzi hao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Joyce Ndalichako .

“Kutokana na mambo yaliyobainika serikali imechukua hatua ikiwemo kuvitaka vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku Saba kuanzia leo, ” amesema.

Amesema vyuo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambazo fedha za mikopo hulipwa ili kuondoa udanganyifu.

“Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa zote za wanafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili,” amesema

Dk. Tulia Afunguka, Asema Ukawa Walimtukana Tusi Kubwa


SIKU mbili baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuahidi kufanyika maridhiano kati ya uongozi wa Bunge na wabunge wa upinzani katika kikao kijacho kinachotarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema hataki kuwasikia wabunge wa upinzani wala kuwawaza.

Kauli hiyo ya Naibu Spika huenda ikazidi kutonesha kidonda hasa baada ya Bunge la Bajeti lililofanyika Mei mwaka huu kuacha majeraha kutokana na wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vyote vilivyoendeshwa na kiongozi huyo.

Juzi wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Azam, Spika Ndugai,  alisema anatafuta mbinu ya kuweka sawa mambo hayo kwa kufanya maridhiano  ikiwemo kushirisha maspika wastaafu.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania juzi katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Tulia alisema hapendi kuwawazia wabunge hao wa upinzani.

“Kwa kuwa Spika yeye kazungumza siwezi kucomment chochote kwa sababu sipendi kuwawazia wabunge hao,”alisema.

Alipoulizwa kwamba ni kwanini migogoro ilizidi wakati yeye akiwa anaendesha vikao, alisema alichokuwa anafuata ni kanuni na kwamba malalamiko hayawezi kukosekana.

“Nashangaa wengine wanasema kuendesha vikao ni mpaka uwe na uzoefu…unajua zile kanuni hata ukipewa uendeshe wewe ukishazielewa hazihitaji uzoefu wowote. Kulalamika kuwa nawapendelea ni jambo la kawaida.

“Kwa mfano siku iliyotokea vurugu wakati wabunge wa upinzani wanadai kutorushwa matangazo ya Bunge live, aliyekuwepo kwenye kiti alikuwa ni mwenyekiti ambaye ni mzoefu wa siku nyingi na ni yeye aliyepeleka majina yao kwenye Kamati ya Maadili, sasa sidhani kama hiyo ni hoja,”alisema Dk. Tulia

Alieleza kushangazwa kwa kitendo cha wabunge wa upinzani katika barua yao waliyomwandikia Spika kwamba hawana imani naye, huku akihusishwa na fedha zilizorejeshwa serikalini.

“Katika ile barua walieleza sababu nyingine kuwa hawana imani na mimi, wakanihusisha na zile Shilingi bilioni 6 zilizorejeshwa serikalini wakati sheria na utaratibu upo wazi kwa sababu Spika au Naibu Spika hauhisiki na masuala ya fedha bali anayehusika ni Katibu wa Bunge.

“Kwa hiyo ni jambo la kushangaza kwamba Naibu Spika karudisha fedha, mimi si mshika mafungu lakini pia ni namna watu walivyopokea huwezi kuwazuia wanavyokuwazia,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Spika Ndugai kwamba kwa kuwa Bunge la 11 lina wabunge wapya wengi na kwamba kuwaongoza kunahitaji uvumilivu mkubwa alisema: “Nisingependa kuongelea kauli ya Spika…lakini uvumilivu wa mtu kutakiwa akae hadi mara 11 halafu ameendelea kusimama ni uvumilivu gani huo?,” alihoji.

Pamoja na mambo mengine alisema wakati wabunge wanawake wa Ukawa walipojitoa kwenye  Chama cha Wabunge Wanawake (TWPG), alitukanwa tusi kubwa lakini alinyamaza.

Mei 5, mwaka huu wakati akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Mbunge wa Ulanga Mashariki, Gudluck Mlinga (CCM), alidai kuwa ili kuwa mbunge wa viti maalumu Chadema lazima uwe ‘baby’ wa mtu.

“Laiti ungeona Hansard tusi walilonitukana siku ile, actually Mlinga hajatukana lakini ulisikia nikilalamika mahali kwamba nimetukanwa? wao wanaongee vibaya…watukane, mimi bado ni kiongozi wao na siwezi kuanza kuwakasirikia itakuwa sasa nashindwa kuwaongoza mimi ni kama mzazi wao,” alisema Dk. Tulia.

Alisema kitendo cha watu kudai kwamba anafanya upendeleo bungeni ni changamoto ya kawaida, kwa sababu hata katika mabunge ya Jumuiya ya Madola malalamiko ya aina hiyo yapo.

“Pale bungeni  wako wabunge 389, hawa ni wengi sana wote hawawezi kupata nafasi ya kuongea. Kwa mfano uliomba nafasi jana ukapewa ukaomba leo, hata ukisimama mara 11 katika hali ya kawaida huwezi kupewa kwa sababu wako wengi ambao hawajachangia.

“Kama kiongozi naona ni sehemu mojawapo ya kusimamia jamii ni changamoto na itaendelea kuwepo kwa miaka mitano,”alisema Dk. Tulia

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wenzake 8 Wafikishwa Mahakamani


Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson Maimu (wa tatu kushoto) na viongozi wengine  nane wa taasisi hiyo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema leo.Habari zaidi tutawaletea.

Mnamo mwezi January 2016, Rais Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6 katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati bado kuna malalamiko kwamba watu wengi hawajapata vitambulisho hivyo. .

Makubaliano ya Simba na MO Dewji kuhusu kuiendesha Simba katika mfumo wa hisa

August 15 2016 kamati ya utendaji ya Simba ilikutana na mfanyabiashara na mkurugenzi mtendaji mkuu wa makampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL) Mohammed Dewji  ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilika na kuanza kuendeshwa klabu hiyo kwa hisa, leo August 17 Simba wametoa makubaliano yao walioafikiana katika kikao chao cha pamoja.
Screenshot_20160817-142506Screenshot_20160817-142425
ALL GOALS:Simba vs URA August 14 2016, Full Time 1-1

Wafanyakazi nane wafukuzwa kazi kisa unene

Habari hii imeripotiwa na BBC ambapo imetokea nchini Misri kwenye television ya Taifa hilo ambapo imewafukuza kazi wafanyakazi 8 wa kike na kuwashauri waende wakapunguze uzito wa mwili.
Chama cha Radio na Televisheni nchini Misri ( ERTU) kimewapa wanawake hao muda wa mwezi mmoja kupunguza uzito kabla ya kuruhusiwa kuonekana tena kwenye television.
BBC
Tangazo hilo limezua lawama kutoka kwa watangazaji walioathiriwa ambapo mmoja wao Khadija Khattab, mtangazaji wa kituo cha Channel 2, amesema kuwa anataka watu ndio watazame kipindi chake na waamue wenyewe ikiwa ana uzito wa juu.

Kauli ya Ibrahimovic iliyofanya atolewe list ya mastaa wa dunia waliowahi kupotezea ofa za Man United

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United Zlatan Ibrahimovic ni moja kati ya wanasoka au watu mashuhuri katika soka wanaoweza kuongea kauli zao za kujiamini kama ilivyo kwa kocha wake Jose MourinhoZlatan aliwahi kusema kuwa hakuna mchezaji anayeweza kukataa ofa ya kujiunga na Man United.
Kauli ambayo ilimfanya August 17 2016 mtandao wa 101greatgoals.com umletee list ya mastaa wa soka wa viwango vya dunia ambao wamewahi kuzipotezea ofa za kujiunga na Man United licha ya kuhitaji na klabu hiyo kwa zaidi ya mara moja.
Screen-Shot-2016-08-17-at-12.18.20
Kauli ya Zlatan “Naamini hakuna mchezaji yoyote anayeweza kukataa ofa ya kujiunga na Man United”
List ya mastaa watano ambao wamewahi zipotezea ofa za kujiunga na Man United
1- Alan Shearer kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson amewahi kujaribu kutaka kumsajili Alan Shearer mara mbili wakati anaondoka Southampton na Blackburnlakini ilishindikana.
2- Usajili wa majira ya joto wa mwaka 2003 ulitawaliwa na jina la Ronaldinho ambaye alikuwa kamaliza mkataba wake na PSG, lakini ndio ilikuwa wakati wa David Beckhamanaondoka Man United, lakini Man United walishindwa kumpata Ronaldinho ambaye alinaswa na FC Barcelona.
Screen-Shot-2016-08-17-at-13.18.02
3- Moja kati ya tetesi kubwa za usajili msimu uliopita ilikuwa ni Sergio Ramos kuhusishwa kwa karibu kujiunga na Man United akitokea Real Madrid, dili ambalo lilikatia njiani na hatimae staa huyo akaendelea na maisha yake ndani ya Real Madrid.
4- Katika kitabu cha maisha halisi ya kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Fergusonamekiri kuwa aliwahi kuhitaji huduma ya kiungo wa zamani wa Liverpool Steven Gerrardlakini mpango wake wa kumshawishi staa huyo ilishindikana.
Screen-Shot-2016-08-17-at-13.25.02
5- Maisha ya Louis van Gaal ndani ya Old Trafford yalikuwa yakihusishwa kwa kiasi kikubwa na kusajili majina ya wachezaji wakubwa kutoka klabu yake ya zamani ya FC Bayern ya Ujerumani, licha Zlatan kuamini kuwa hakuna mchezaji anayeweza kukataa ofa ya kujiunga na Man United, Thomas Muller aliipotezea ofa ya Man United.
Screen-Shot-2016-08-17-at-13.27.43

Azam FC waifunga Yanga na kutwaa Ngao ya Hisani

Mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara 2016/17 ambao ulifanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ulipigwa mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2015/2016 Young Africans na mshindi wa pili wa Ligi Kuu Azam FC hiyo ikiwa ishara ya kukaribia kuanza kwa msimu mpya wa Ligi.
IMG_0391
Mabingwa wa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga SC imenyang’anywa Ngao ya Jamii na Azam FC baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 2-2 katika mchezo huo.
IMG_0401
Mshambuliaji Donald Ngoma alikuwa wa kwanza kupata goli la kwa mkwaju wa penati na dakika 2 baadae kuongeza goli la pili kwa kutumia vyema pasi ya Amissi Tambwe, Dakika ya 74 Shomari Kapombe aliipatia Azam bao la kwanza akitumia makosa ya mabeki wa Yanga John Bocco ‘Adebayor’ aliisawazishia Azam kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 penati iliyotokana na beki wa Yanga kuushika mpira kwenye box.

Young Killer akaribisha watakaomsaidia kuandika mashairi

Young Killer amefungua milango kwa mwandishi yeyote anayeweza na mwenye nia ya kumwandikia wimbo utakaokuwa kwenye level zake.
Young Killer
Pia amekaribisha producer yeyote mchanga mwenye uwezo wa kutengeneza midundo mikali.
Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa huu ndio muda muafaka kwakuwa hakuwahi kuandikiwa nyimbo hapo kabla na mashabiki tayari wameshaufahamu uwezo wake mkubwa alionao kwenye sanaa.
“Nishaonyesha uwezo mkubwa na sikuwahi kuandikiwa nyimbo hata siku moja toka nimeanza,” amesema. “Sasa nafungua dirisha la usajili kwa yeyote anayetaka kuniandikia ngoma kali iwe na uwezo ambao mkubwa kama au zaidi na pia nakaribisha maproducer hata akiwa mchanga lakini ana uwezo ambao anaona utafanana na mimi namkaribisha,” amesisitiza.
Wiki hii rapper huyo aliachia ngoma mpya iitwayo Mtafutaji.

Miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta wakipata tabu na hata kufanya upasuaji hatari ili kuongeza makalio na wengi wameharibika kabisa au kupoteza maisha kwenye oparesheni hizo hatari. lakini kama jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo kitaalamu inaitwa gluteal maximus, gluteal minimus na gluteal medias.

Hiyo ndio misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi vizuri huongezeka na kua mikubwa. ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha mwili chenye misuli lakini sio kua makubwa tu lakini hata kuyafanya kua na shepu nzuri na kuvutia.. unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..

1. Mazoezi ya squat;
mazoezi haya huanzwa kwa kusimama na miguu yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka, mazoezi haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku za kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo zimeanza kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza makalio.fanya zoezi hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na tano au unaweza ukaanza kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja kisha ukaendelea na mazoezi ya kawaida kama nilivyoelekeza.
2. Zoezi la bridge;
watu wengi wanashinda wamekaa kwenye viti  mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata mtu mwenye makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno kwa juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa mbele kwa sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya hivi kwa kila mguu mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika mbili kila baada ya raundi.

3. Donkey kick;
piga magoti kisha weka mikono chini kama mbuzi anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu kisha rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na kuurudisha mara 20.

4. Kula protini nyingi:
vyakula vya protini ni muhimu kujenga misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa, karanga, korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.

5. Chagua aina nzuri ya wanga;
ulaji wa mikaango kama chips, chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta vitambi na kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.

6. Tumia mboga za majani; 
mboga za majani ni muhimu sana kwani husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na mwili kirahisi na kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.

 7. Tumia virutubisho vya kutosha;
virutubisho vyenye madini mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja kwa moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha wanaotumia virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia kabisa.jinsi ya kutumia; chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye virutubisho vyako kisha changanya na maziwa kwa upande wa protein shake na kwa upande wa argi changanya kijiko kimoja cha unga na maziwa ya mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku huku ukiendelea na mazoezi.

Mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua muda angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na haimaanishi kwamba ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana, mazoezi ni muhimu kwa mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la mwezi yaani mara moja kwa siku kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa wiki baada ya mwezi wa kwanza. kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi kufanikiwa, usije ukafanya zoezi siku mbili ukaacha afu ukategemea mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata virutubisho hivyo, kupata video za mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu zaidi.